Kila mmoja alikuwa na lake la kusema, wengine
walithubutu kutamka kuwa bora Real Madrid wamekufa kiume ingawa kipigo ni
kipigo.
Barcelona wameaga michuano ya Ligi ya Mabingwa mwaka
huu kwa aibu ambayo itabaki katika historia yao kwa kipindi kirefu baada ya
kufungwa jumla ya mabao 7-0.
Mabao 4-0 mjini Munich na 3-0 ndani ya Camp Nou, ni
aibu ya aina yake, mbaya zaidi wageni Bayern walionekana kuutawala zaidi
mchezo.
Mabao ya Bayern yalifungwa na Robben, Pique
akajifunga na Muller akamalizia la tatu.
Lionel Messi ambaye ni sawa na mkombozi alikuwa
kwenye benchi akiishuhudia Barcelona ikiumizwa nyumbani na Wajerumani hao.
Mara kadhaa, Aarjen Roben na Frank Ribery wa Bayern
ndiyo walionekana kuwa matatizo makubwa kwa beki ya Barcelona iliyoongozwa na
Gerard Pique.
Wakati washambuliaji wa Barcelona walioongozwa na
David Villa walikuwa wachovu na wasio tishio hata kidogo.
Ajabu Barcelona waliamua kuwatoa viungo wao tegemeo
Iniesta na Xavi ikiwa ni dalili ya kukubali matokeo mapema.
Munich imesonga fainali, sasa inakutana na
wapinzani wake wakubwa katika Bundesliga, Borussia Dortmund ambao wamewavua
ubingwa hivi karibuni.
Dortmund walisonga baada ya kuitoa Real Madrid kwa
jumla ya mabao 4-3 ikiwa walishinda kwao kwa mabao 4-1 na baadaye wakapoteza
jana kwa kuchapwa 2-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment