Pamoja na Real Madrid kutolewa katika nusu fainali
ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 4-3, Cristiano Ronaldo amesema
anabaki.
PSG na Man United zilionyesha nia ya kumtaka
mshambuliaji huyo aliyetua Madrid akitokea Man United iliyomnasa akiwa kinda
tokea Sporting Lisbon ya Ureno.
“Nina mkataba wa miaka miwili, sina hofu na ninaona
nina furaha. Nitabaki kuendelea kupambana kupata makombe,” alisema Ronaldo.
Kauli hiyo inaonekana kuwa tata, bado haieleweki
kama amesema akiwa amemaanisha kweli au baadaye ataondoka zake kutokana na
taarifa za mwanzo zilizokuwa zikieleza anataka kurejea United.
Tayari Kocha Mourinho anaonekana ataondoka na kutua
Chelsea, klabu yake ya zamani ambayo alifanya vizuri akiwa hapo.
0 COMMENTS:
Post a Comment