Kipigo cha jumla ya mabao 7-0 ilichotoa Bayern
Munich kwa Barcelona ni kikubwa kuliko vyote vilivyowahi kutolewa katika Ligi
ya Mabingwa hatua ya nusu fainali.
Bayern ilishinda kwa mabao 4-0 nyumbani na 0-3
ugenini, maana yake ndiyo ushindi mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika michuano
hiyo katika nusu fainali.
Barcelona ambao walikuwa nyumbani, walicheza
kichovu na hawakuonyesha kama kweli wangeweza kurudisha mabao manne waliyofungwa
na kufunga la tano.
Badala yake, wageni ndiyo walionekana kama
wamepoteza mchezo wa kwanza na walitaka kufunga mabao mengine.
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya sasa ni ya
Wajerumani tupu na itachezwa Mei 25 kwenye Uwanja wa Wembley jijini London, England.
Bayern inakutana
na wapinzani wao Borussia Dortmund ambao wana hasira ya kupokonywa ubingwa wa
Bundesliga.
0 COMMENTS:
Post a Comment