Kiungo mshambuliaji wa Simba,
Amri Kiemba amesema yupo tayari kurejea katika klabu ya zamani ya Yanga.
Kiemba anasema yuko tayari
kusaini katika klabu yoyote inayoshiriki Ligi Ligi Kuu Tanzania Bara hata kama
ni Yanga.
Mkataba wa Kiemba na Simba,
unamalizika mara baada ya msimu huu ambao umebaki mechi mbili tu.
Maana yake Kiemba anaweza
kuzungumza na timu yoyote kwa mujibu wa sheria za usajili za Shirikisho la Soka
la Kimataifa (Fifa).
Hivyo Yanga na timu nyingine
zinaweza kuzungumza na kiungo huyo ambaye ameonyesha uwezo mkubwa hasa msimu
huu.
Awali ilionekana kama Kiemba
alikuwa amepoteza mwelekeo, lakini kutua Simba kwa Kocha, Milovan Cirkovic raia
wa Serbia kulimrejesha katika kiwango cha juu.
Kiemba alicheza Yanga wakati
ikiwa chini ya Kocha Jack Chamangwana raia wa Malawi. Lakini amewahi kukipiga
Miembeni ya Zanzibar kabla ya kurejea Bara na kujiunga na Moro United.
0 COMMENTS:
Post a Comment