Kocha Mkuu
wa Yanga, Ernie Brandts amesema kikosi chake dhidi ya Coastasl Union
kitawashangaza wengi leo.
Yanga
inaivaa Coastal leo saa 10 jioni katika mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo itakuwa
ni ya pili kutoka mwisho kwa Yanga. Baada ya mechi hiyo ifatunga msimu na
Simba.
Tayari
Yanga ni mabingwa baada ya Coastal Union kutoka sare ya Azam FC mjini Tanga
wiki iliyopita.
Brandts
alisema mechi hiyo atatoa nafasi kwa wachezaji kadhaa ambao hawajawahi kupata
nafasi.
“Njoo uone,
kutakuwa na mabadiliko makubwa na kikosi kitawashangaza wengi,” alisema.
Kabla ya
hapo, msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto aliiambia Salehjembe kwamba uwanjani
kutakuwa na ‘sapraiz’.
“Njooni
muone, ni bonge la sapraiz,” alisema Kizuguto.
Brandts
anategemea kuwapumzisha wachezaji wake sita ambao wana kadi za njano ambao ni
pamoja na kipa, Ally Mustapha ‘Barthez’, Athuman Idd ‘Chuji’, Simon Msuva,
David Luhende, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza ili kuepuka wasiikose mechi ya
Simba kama watalambwa kadi nyingine ya njano ambayo itakuwa ya tatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment