Roberto
Mancini amefukuzwa kazi siku moja baada ya kutimiza mwaka mmoja baada ya kutwaa
ubingwa wa Ligi Kuu England.
Kutokana
na kufukuzwa huko katika mtindo ulioonekana ni wa kikatili, Mancini atalipwa
pauni milioni 7 kwa kuwa mkataba wake na klabu hiyo ulikuwa na miaka mitatu
mbele.
Mancini
raia wa Italia ameiwezesha Manchester City kutwaa Kombe la Ligi Kuu England na
lile maarufu la FA.
Kocha
huyo alipata taarifa za kufutwa kwake kazi dakika chache baada ya kutoka
mazoezini kujiandaa na mechi dhidi ya Reading. Mmoja wa Wakurugenzi, Ferran
Soriano ndiye alimueleza lakini ikaelezwa baadaye akazungumza na bosi mwenye
timu, Mwenyekiti Khaldoon Al Mubarak ambaye yuko Abu Dhabi.
Taarifa
zinaeleza, tajiri huyo mwarabu hakupenda kumfukuza Mancini lakini baada ya
kufungwa katika fainali ya Kombe FA kwa bao 1-0 na Wigan, asilimia kubwa ya
wakurugenzi walitaka aondolewe.
Pellegrini,
59, ndiye anaonekana ni chaguo la Man City ingawa tayari kocha huyo amezungumza
kwamba hana mpango huo.
Imeelezwa
kumekuwa na taarifa za kutaka kujiunga na Barcelona ambayo ina hofu na afya ya
kocha wake, Tito Vilanova anayetibiwa ugonjwa wa kansa.
Tayari
Man City wako tayari kumtwaa kwa Pellegrini kutoka Malaga kwa kulipa pauni
milioni 3.3 ili kuvunja mkataba wake na mazungumzo yamekuwa yakiendelea.
Baada
ya kutimuliwa kwa kocha huyo aliyekuwa mshindani mkubwa wa Alex Ferguson,
mashabiki wa Man United walionekana mtaani wakiwa na mapango yaliyokuwa yenye
maandishi yanayotaka “akapumzike kwa amani” huku kukiwa na picha za Ferguson
kuonyesha wanamkubali zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment