Baada ya
kuifunga Simba kwa mabao 2-0, Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts anatarajia
kuondoka leo kwenda kwoa Uholanzi.
Brandts
anakwenda Uholanzi kwa mapumziko baada ya msimu wa Ligi Kuu Bara kufikia tamati.
Kocha huyo
ameiambia Salehjembe kwamba atakaa Uholanzi kwa wiki kadhaa kablaya kufanya
safari ya mapumziko nje ya nchi hiyo.
“Nitakaa
nyumbani kidogo, baadaye nitakuwa na safari ya mapumziko na familia,” alisema.
Alisema anatarajia
kurejea nchini baada ya wiki kadhaa, tayari kuanza maandalizi ya kikosi chake.
Brandts
ameingoza Yanga kutwaa ubingwa wa Bara ikiwa ni pamoja na kuwafunga watani wao
Yanga katika mechi ya mwisho ya ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment