Mlezi wa
Simba, Rahma Al Kharusi amesema amesikitika kuikosa mechi ya watani, Yanga na
Simba iliyopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa.
Rahma
maarufu kama Malkia wa nyuki, amesema alipania kuja nchini kuiona mechi hiyo
lakini ilishindikana.
“Nilibanwa
na majukumu kadhaa yakiwemo mengine ya kiserikali hapa Oman, hivyo nikashindwa
kuja.
“Najua
Simba wamepoteza mchezo, lakini bado nasisitiza lazima Simba tujipange kwa
ajili ya msimu ujao. Tayari wenzetu Yanga walikuwa vizuri, hivyo hatuna jana ya
kusikitika sana.
“Tuangalie
programu yetu ni nini na kitu gani cha maana ambacho tunafanya,” alisema.
Malkia wa
nyuki ndiye amekuwa nguzo ya Simba kwa kushirikiana na kundi la Friends of
Simba kuhakikisha klabu hiyo inarudisha heshima yake baada ya kuwa imeyumba
chini ya uongozi wa Aden Rage.
0 COMMENTS:
Post a Comment