May 21, 2013



 
Kocha wa zamani wa Yanga, Milutin Sredojevich ‘Micho’ ndiye kocha mpya wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.

Micho raia wa Serbia, amepewa kazi ya kuinoa timu hiyo baada ya kuwashinda makocha lukuki akiwemo mwingine wa zamani wa Yanga, Tom Saintfiet raia wa Ubelgiji.

Micho amepata nafasi hiyo ikiwa ni siku chache tokea atimuliwe kuinoa timu ya taifa ya Rwanda, Amavubi ambaye ilishindwa kufanya vizuri katika michuano ya awali kucheza Kombe la Dunia.


Akizungumza na Salehjembe, Micho alisema yuko katika wakati ambao kuna mambo anapaswa kumalizia na baaye atafunguka na kueleza kila kitu.

“Hilo suala si sasa hizi, kuna mambo namalizia, halafu nitaweza kuzungumza,” alisema Micho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic