Kocha Mkuu mpya wa Uganda, Sredojevich Milutin ‘Micho’
amesema atafanya makubwa akiwa na kikosi hicho maarufu kama The Cranes.
Micho raia wa Serbia, ambaye hivi karibuni ametimuliwa kuinoa Rwanda, Amavubi amepewa nafasi ya kuinoa
Uganda na atakuwa akisaidiwa na kocha mwingine wa zamani wa Yanga, Sam Timbe.
Micho amesema anaamini Uganda ni sawa na nyumbani
kwa kuwa alifanya kazi kwa kipindi kirefu wakati akiinoa SC Villa, hivyo
aliamini siku moja angerudi.
Akizungumza na Salehjembe kutoka Kampala, Micho
alisema anatamani kuanza kazi hata leo.
“Hapa nimerudi nyumbani, natamani nianze kazi hata
leo. Lakini kitu kikubwa ambacho ninaamini nitafanya vizuri na Uganda.
“Najua soka la Uganda, nawajua wachezaji pia najua
Waganda wanataka ushindi na wako tayari kuisaidia timu yao ya taifa.
“Hivyo kila kitu kitakwenda vizuri kama wote kwa
pamoja tukitaka wafanye hivyo,” alisema Micho.
“Awali nilitaka kuja Tanzania kuangalia mechi ya
Yanga na Simba, lakini nilishindwa kutokana na kuwa katika mazungumzo ya mwisho
na Fufa.
“Bado naendelea kuwashukuru watu wa Rwanda, hasa
walioshirikiana nami, lakini nguvu zote nazielekeza katika kazi mpya.”
Micho aliwahi kuinoa Yanga wakati ikishiriki Ligi
Ndogo mwaka 2008, Timbe pia alikuwa kocha wa Yanga mwaka juzi na kuipa ubingwa
wa Kombe la Kagame.
0 COMMENTS:
Post a Comment