May 31, 2013



Msanii M To The P bado anaendelea kuhoji alipo rafiki yake Albert Mangweha ‘Mangwea’.

Tokea amepata fahamu, M To The P amekuwa akitaka kujua aliko rafiki yake kipenzi.

Lakini wengi we mekuwa wakijitahidi kumuambia kuwa ameondoka kwenda Dar es Salaam hivyo akipona atamkuta.

“Jamaa anataka kujua kwamba Mangwea yuko wapi, hivyo inabidi tujaribu kumdanganya maana kama tutamuambia, tunahofia anaweza kuumwa zaidi,” alisema Joseh mmoja wa Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini.

Kauli hiyo ya Mangwea ameishatangulia Bongo, alielezwa hata aliposikika akihojiwa moja kwa moja na mtangazaji Millard Ayo wa Clouds Fm ambaye yuko jijini Johannesburg.

M To The P alimuambia Millard kuwa anasumbuliwa na kifua na kukosa nguvu huku akiwaomba Watanzania wamuombee dua.
 
Mangwea na M To The P walikutwa wakiwa taabani hawajitambui chumbani, lakini baadaye Mangwea alipoteza maisha na M To The P kulazwa akiwa hajitambui kwa zaidi ya siku mbili hali iliyosababisha azushiwe kifo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic