May 31, 2013



 
Kocha wa timu ya taifa ya Italia, Cesare Prandelli ametaka mshambuliaji wake Mario Balotelli aachwe apumzike.

Prandelli amesema Balotelli amekuwa akisakamwa mfululizo na kumfanya ashindwe kufanya mambo yake vizuri.


Kocha huyo alilizungumzia sakata la Balotelli kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya na kundi maarufu linalofanya biashara hizo la Neopolitan Camorra.

Kundi hilo pia hujihusisha na matukio ya utekaji na kuuwa watu na wakati fulani Balotelli aliwahi kulishambulia bila ya uoga.

Prandelli alisema haamini Balotelli anaweza akajihusisha na uuzaji madawa ya kulevya, badala yake wanaofanya hivyo wamegeuza kama mazoea kumsakama.

Kwa upande wake, Balotelli alionekana kutojali na badala yake alionekana mtaani akiranda na mrembo wake, Naguesha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic