May 24, 2013


Mbogo dakika chache kabla ya upasuaji wa kwanza katika hospitali ya Mwananyamala..


Beki wa kati wa Yanga, Mbogo Ladislaus anatarajia kurejea tena katika chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa tena upasuaji.

Mbogo alifanyiwa upasuaji wa kwanza kwa ajili ya kutoa uvimbe katika shavu lake.

Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya amethibitisha kuwadia kwa wakati kwa ajili ya upasuaji kwa mara ya pili.


“Kweli, mipango imeanza na wiki ijayo Jumanne atakwenda clinic kuangalia nini cha kufanyika halafu upasuaji utafuata,” alisema Matuzya.
Tayari Mbogo alishaanza mazoezi baada ya upasuaji wa kwanza kwenda vizuri na kwa mafanikio.

Upasuaji wa pili unatakiwa kufanyika kwa ajili ya kusaidia kuondoa ngozi ili kumpa muonekano mzuri.

Beki huyo alijiunga na Yanga akitokea Toto ya Mwanza, hata hivyo amekuwa katika wakati mgumu wa kupigania namba dhidi ya Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic