Carteron akisaini mkataba wake na mmiliki wa Mazembe, Katumbi |
Kocha mpya
wa TP Mazembe, Patrice Carteron raia wa Ufaransa amesaini mkataba
wa miaka miwili lakini utambulisho wake umezua balaa baada ya mtu mmoja
kufariki dunia.
Kocha huyo wa zamani wa Mali, bado ataendelea
kufanya kazi yake hiyo ya sasa kabla ya kurejea na kuanza kazi yake na TP
Mazembe.
Baada ya kusaini mkataba na mmiliki wa
Mazembe, Moise Katumbi alipelekwa kutambulishwa na watu walijitokeza kwa wingi
sana uwanjani.
Hali iliyosababisha msongamano mkubwa hadi
kufikia mtoto mmoja kukanyagwa hadi kupoteza maisha, kitu ambacho kimeelezwa ni
pigo kwa mashabiki na jamii ya Lubumbashi.
Katumbi ambaye pia ni gavana wa jimbo hilo,
tayari ametoa pole kwa familia ya mtoto huyo na Mazembe wameshiriki mwanzo hadi
mwisho wa msiba huo.
Siku ya tukio hilo, kocha huyo mgeni
aliishuhudia timu yake mpya ikiichapa Muungano kwa mabao 3-0 huku Mtanzania
Thomas Ulimwengu akifunga bao moja.
Carteron amechukua kazi ya Lamine N'Diaye raia wa Senegal aliyeamua kujiuzulu baada ya timu yake kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment