May 5, 2013



Short akiwa na Malkia wa nyuki katika ndege yake ya kifahari baada ya kufika uwanjani kuwapokea walipowasili mjini Newcastle jioni ya leo wakitokea London...
Na Mwandishi Wetu
MMILIKI wa klabu ya Sunderland, Ellis Short amewafanyia kufuru ya jeuri ya fedha Mlezi wa klabu hiyo, Rahma Al Kharusi ‘Malkia wa Nyuki’ kwa kumpa ndege binafsi kama usafiri.

Pamoja na kupewa ndege hiyo ambayo mamilionea wa Uingereza huzitumia kwa usafiri binafsi Malkia wa nyuki atakuwepo uwanjani kesho usiku usiku katika viti maalum vya watu matajiri wakati Sunderland na Kocha Roberto Di Canio watakapokuwa wanawavaa Stoke City katika Ligi Kuu England wakipambana kukwepa kuteremka daraja.


Short ambaye ni mmoja wa mamilionea wa Uingereza, ametoa ndege yake binafsi ya kifahari na kumkabithi Malkia wa nyuki asafiri nayo kutoka London hadi Newcastle ambako atakutana naye.

Tayari Short amefika kwenye uwanja wa ndege Newcastle leo jioni na kumpokea Malkia wa nyuki ambaye imeelezwa baadaye aliungana na Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage watakayekuwa pamoja kuanzia leo.
 
Short, Malkia wa Nyuki na binti yake, Fatma..
Wakiwa na ndege hiyo walisafiri kwa zaidi ya kilomita 486 wakiwa angani kabla ya kutua Newcastle na kukutana na Short.

 “Kweli malkia ataondoka leo kutoka London kwenye Newcastle kwa ajili ya kukutana na mmiliki wa Sunderland ambaye alimualika kwenda huko.


“Lakini mwenyekiti Rage naye yuko hapa London na ataondokana naye kwa njia yake hadi sehemu ambayo watapandia ndege na pale ndiyo ataungana na Malkia wa nyuki, wote watapanda ndege hiyo ya Short kwenda Newcastle,” kilifafanua chanzo.

“Wakiwa Newcastle, kwa pamoja watakutana na Short na kufanya naye mazungumzo kuhusiana na suala la kuanzisha uhusiano lakini pia kuhusiana wa klabu hizo mbili.”

Lakini jioni hii, Salehjembe, imefanikiwa kumpata Malkia ambaye amesema wamewasili mjini humo tayari kwa mazungumzo.

“Kila kitu kinakwenda vizuri, tunatarajia kuwa na mazungumzo ha Short na lengo ni manufaa ya Simba. Pamoja na hivyo tumealikwa kwa ajili ya mechi ya vijana ambayo Sunderland watachezaji kesho Jumatatu asubuhi.

“Lakini usiku kutakuwa na mechi ya Ligi Kuu England watakayocheza dhidi ya Stoke City. Tumealikwa pia na mazungumzo yetu pia yatafanyika.

“Kwa kuwa ndiyo nimefika, nafikiri nitazungumza wakati mwingine acha nijiandae na ratiba ingawa hadi sasa kwa niaba ya Simba namshukuru sana Short kwa kuwa ametupokea vizuri na tulisafiri na ndege yake kutokea London,” alisema Malkia wa nyuki.

Lengo ni kuanzisha uhusiano na kusaidiana katika masuala kadhaa yakiwemo ya ushauri wa kifundi na mengine.
Awali Simba iliwahi kutumia jina la Sunderland kabla ya kubadilisha mengine kadhaa na kuwa Simba ambalo linatumika hadi leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic