February 23, 2020


Mpira umemalizika Uwanja wa Mkwakwani Tanga
Coastal Union 0-0 Yanga

Yanga inagawana pointi moja na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Kipindi cha pili kimeanza Uwanja wa Mkwakwani Tanga
Ziliongezwa dakika nne kukamilisha kipindi cha kwanza

Dakika ya 16 Ayoub Lyanga alikosa nafasi ya wazi akiwa na mlinda mlango Metacha Mnata

Dakika 15 za kipindi cha kwanza mechi ilikuwa ni sawa kwa timu zote mbili kutengeneza nafasi na kushindwa kuzitumia.

Dakika ya 12 Bernard Morrison alipiga kona ambayo haikuzaa matunda UWANJA wa Mkwakwani, Coastal Union imeikaribisha Yanga leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Yanga mchezo wa kwanza ilishinda bao 1-0 ulichezwa Uwanja wa Uhuru hivyo leo ni mpira wa kisasi kwa Coastal Union na kulinda rekodi kwa Yanga,

14 COMMENTS:

  1. Wapingwe yebo yebo hao vyura

    ReplyDelete
  2. Yanga kashinda kwa matokeo ya sare.Tunangoja maandamano.

    ReplyDelete
  3. Wakale walisema Samaki Akioza usimtupe, umtafutie viungo umkaushe. Pupa zetu za kumtimua Zahera ndizo zilizotuvuruga tukafika hali hii tuliyokuwa nayo

    ReplyDelete
  4. Zahera atasema, mlikuwa hamnijui na mkatafuta mwengine. Hali nzuri ya pesa tuliyokuwa nayo kwa sasa basi kwa Zahera angetufikisha mbali, lakini Wapiiiii. Mitaani hakukaliki kwa vicheko

    ReplyDelete
  5. Samaki akioza kweli usimtupe nitafutie viungo.Je akioza chura?🤔🤔🤔

    ReplyDelete
  6. Mpira siku hizi ni biashara na inahitaji mipango endelevu kama zilivyo biashara nyingine. Propaganda haziwezi saidia hata siku moja na hakuna mtu atawekeza hela yake bila ya kujuwa atapataje faida. Yanga hata aje Gudiola kwa utaratibu wa kudanganyana eti timu ya wananchi wakati wanufaika ni wachache haiwezi fika kokote. Hiyo ni sawa na maskini anavyojifariji kwa umaskini wake kwamba mwenzake tajiri ni free masons!!! Hahaha wakikosa hela wanajita wananchi na wakipata vimisaada wanajiita Young Africans wataleta mpaka wazungu uwanjani na kujiona wanamashabiki waliyostaarabika huku wananchi wenzao wakiwaita vibaka! Na wakikosa ubingwa wanajiita Mabingwa wa JADI sasa sijui wanacheza ngoma za jadi!!! Bila mabadiliko ya kweli itabaki kiliyo tu huku wachache wakiendelea kunufaika. Acha tujifariji kidogo SIMBA wanabebwa hahaha ama kweli akili ni nywele.

    ReplyDelete
  7. Ili kuwakomoa Simba walikuwa wanaomba wachezaji wa kigeni kwa pesa za GSM na baada ya mwezi huwatimua na kuzoa wengine ni haya ndiyo yaliyowavuruga wa matopeni

    ReplyDelete
  8. Wao kila wafanyalo Simba siku yapili nao wanaiga. Simba wameleta mtaalamu nao haraka wakamleta wao na Kuanza kumsifu kabla ya Kuanza kazi na Simba walipomtimuwa kocha mzungu nao haraka wakamtimuwa Zahera. Vurugu na ubabe na sasa wamenyewa kimya wanaitazama arjojo itaangukia wapi

    ReplyDelete
  9. Na wameshatamka wamo mipango ya kuleta mchezaji na kufukuza mwengine

    ReplyDelete
  10. Yanga basi ni kujaza ratiba ya mechi tu ...hakuna la kusema ..wamezama sasa

    ReplyDelete
  11. Bado mpaka abakishe mechi kumi ndio MISSION ITAKUA COMFIRMED,walikua wanajisifu sana hawa jamaa kumbe dah mipango hewa tu,mungu awahurumie sana,na bado kivumbi kutoka simba,kutoka azam,kutoka namungo,na wengine kibao ambao hajarudiana nao ugenini.mnabebwa mpaka aibu,kwanini goli la polis tanzania lilikataliwa?alafu mnageuza eti simba inabebwa lipuli mmewazulumu goli sasa hayo ndio malipo ya dhuluma zenu na bado mbona,na labda mkimbie maana deo kanda ameshapona na ameshaanza mazoezi mtachezea goli nyingi sana round hii tuna hasira na nyinyi sana.

    ReplyDelete
  12. Kwanza mechi ya jana wamechezesha mchezaji ambaye hayupo kwenye listi ya wachezaji wa akiba. Mchezaji mwenyewe ni Kampamba kutoka Zambia.Hakuwepo kwenye lusi ya wachezaji 7 wa akiba.

    ReplyDelete
  13. Sorry kocha hewa bora achukuliwe Dkt Shika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic