Mtanzania Yona Elias Ndabila amezua jambo nchini
Nepal baada ya timu yake ya Sarswoti Youth Club kugomea usajili wake.
Pamoja na timu kubwa ya Manange kuamua kutoa dau
kubwa ambalo hata hivyo halijawekwa wazi, uongozi wa Sarswoti uligoma.
Mjadala huo ulikuwa mkubwa na kuzua gumzo katika
soka nchini humo lakini mwisho Manange imefanikiwa kumnasa Ndabila,
mshambuliaji wa zamani wa Prisons na Mtibwa Sugar.
Rais wa Manange, Jamling
Ghale amethibitisha kuwa Ndabila ameishamwaga wino katika timu hiyo.
Salehjembe ilikuwa ya kwanza
kueleza kuhusiana na Ndabila kujiunga na timu hiyo kabla ya tafrani hilo la
usajili.
Ndabila amesema tayari yuko
katika kambi ya timu yake mpya na anafanya mazoezi kwa juhudi kujiandaa na
michuano ya Gurkha Cup.
Msimu uliopita wa ligi ya
Nepal, Ndabila alishika nafasi ya pili kwa kupachika mabao baada ya kufunga 17
lakini alifanikiwa kupachika sita pekee walipokutana na timu ya Bansbari.
0 COMMENTS:
Post a Comment