Waliokuwa mabingwa wa Tanzania Bara, Simba wametua
mjini Unguja na wapishi wao mjini Unguja kwa ajili ya kambi.
Simba imetua Unguja tayari kujiwinda kwa mechi yao
dhidi ya Yanga, Mei 18 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga inajiandaa kucheza na Yanga katika mechi
ambayo tayari joto lake limepanda kwa kasi ya kimondo.
Uamuzi wa Simba kutua na wapishi wake Unguja
inaonekana ni hofu ya kuwa na hujuma.
Lakini Kocha Mkuu, Patrick Liewig akasema huo ni
sehemu ya mfumo wa wao kutaka kujitegemea zaidi na wachezaji wao kupata
wanachotaka.
“Ni kitu cha kawaida kabisa, hakuna haja ya kuanza
kufikiria kuhusiana na hujuma.
“Hata kama ingekuwa hivyo, hakuna ambaye angeweza
kupata nafasi ya kutuhujumu na tunajiandaa vizuri kabisa,” alisema Liewig.
Simba iko katika nafasi ya tatu wakati Yanga tayari
ni mabingwa na Azam FC iko katika nafasi ya tatu.
Mechi hiyo kwa Yanga ni sehemu ya kutaka kulipa
kisasi baada ya kumaliza msimu uliopita kwa kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa
Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment