Nyota wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi bado
anaendelea kupambana kupata namba katika kikosi cha kwanza cha timu yake mpya
ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Pamoja na benchi la ufundi kuonyesha kumkubali, lakini
bado halijamuamini kiasi cha kumpa nafasi 11 za kwanza kikosi kinachopangwa.
Tayari Okwi raia wa Uganda ameshafunga bao moja
maridadi katika mechi moja lakini bado linaonekana halijatosha kulishawishi
benchi hilo la ufundi.
Lakini Okwi amendelea kufanya mazoezi kwa juhudi na
huenda wanaamini atapata nafasi hapo baadaye.
Ushindani wa namba katika kikosi hicho uko juu,
ingawa Okwi anaweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza kama ataendelea
kupambana.
Aliondoka nchini akiwa tegemeo la Simba na namba
katika kikosi cha kwanza haikuwa na maswali hata kidogo.
Simba ambayo pamoja na kumkosa, inaendelea kudai
fedha zake dola 300,000 ilizomuuza kiungo huyo mshambuliaji kwa Waarabu wa
Tunisia bila ya mafanikio.
0 COMMENTS:
Post a Comment