Shekhan, kushoto akiwa mazoezini na Kilimanjaro Stars, kulia ni William John aliyewahi kucheza Simba... |
Kiungo nyota wa zamani wa Simba, Shekhan Rashid
amewaonya Simba kutokana na mwenendo wanaokwenda nao.
Shekhan ambaye anaishi jijini Stockholm, Sweden
amesema Simba inaweza kubadilika na kuwa bora lakini kama uongozi
utajirekebisha na kuendesha mambo vizuri.
Pamoja na hivyo, kiungo huyo ambaye alikuwa
anasifika kwa kupiga pasi ‘rula’ amesema ushirikiano na kupendana baina ya
wachezaji kutaifanya Simba irejee katika hali yake.
“Mimi niko mbali huku, lakini ninaamini kama
uongozi utafanya kazi yake vizuri, basi mambo yatakwenda vizuri tu na Simba
itarudi katika hali yake.
“Lakini suala la umoja, upendo kati ya wachezaji,
benchi la ufundi na wote wanaohusika na timu ni kitu muhimu sana,” alisema
Shekhan ambaye ni baba wa watoto wawili.
Je, unataka kujua anafanya nini nchini humo,
anaendelea na soka au maisha yake yako vipi? Soma baadaye makala inayohusu
maisha yake na kila kitu kuhusiana na kiungo huyo nyota wa zamanio wa Wekundu
wa Msimbazi ambaye alianzia Yanga ambao walimdharau, akatua Simba na kutisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment