Yanga waliahidi watakuwa na sapraiz leo kwenye
uwanja wa taifa na haijawahi kutokea katika soka la Bongo.
Kumbe walichopanga kufanya ni hiki, hata kabla ya
wachezaji kupasha misuri, walizunguka uwanja wakiwapigia makofi mashabiki wao.
Wachezaji pamoja na safu nzima ya benchi la ufundi
ilifanya hivyo kuonyesha shukurani kwa mashabiki waliowasapoti hadi kutwaa
ubingwa.
Lakini pamoja na kufanya staili hiyo mpya ya ‘kisasa’,
Yanga hawakuthubutu hata kidogo kupitiliza upande wa pili wa uwanja ambako kuna
rangi nyekundu na nyeupe.
Ilionekana huenda ‘watatia maguu’ kuwashukuru
watani wao ambao walikuwa wakihudhuria mechi zao nyingi tu. Lakini wapi,
walipokaribia tu upande wa pili, sauti zikaanza kupazwa zikionyesha kwamba
wasingependa wafike upande huo.
Yanga nao wakaonyesha wala hawakuwa na mpango wa
kuvuka hadi anga za watani, hivyo wakakata kona na kurejea upande wao huku
wakishangiliwa na mashabiki wao waliokuwa wamesimama na kuwapigia makofi kujibu
walichokuwa wanakifanya.
Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa ikiwa na mechi
mbili mkononi, hiyo ya leo dhidi ya Coastal Union na ile la Mei 15 dhidi ya
watani wao Simba ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment