May 31, 2013


BOBAN, KULIA AKIWA NA KINJE


Pamoja na wakala mmoja wa Qatar kuvutiwa na Haruna Moshi ‘Boban’ na kumshawishi ampeleke kucheza soka nchini humo, klabu ya Sofapaka ya Kenya imeingilia kati.

Sofapaka inayomilikiwa na Elly Kalekwa kutoka DR Congo, imeanza mazungumzo na Boban ikiwezekana ndani ya siku chache atakuwa mchezaji wao rasmi.

“Sasa hatuwezi kuzungumza sana, ila Boban ameonyesha yuko tayari kucheza kwetu kama tutamuongezea maslahi kama alivyotaka.

“Tumekuwa tukimfuatilia kwa karibu sana na uwezo wake umekuwa ni wa kuridhisha. Hivyo inawezekana akaungana nasi,” alisema mmoja wa maofisa wanaoshukughulikia usajili kwa upande wa Sofapaka.

Boban amemaliza mkataba wake na Simba ambayo tayari imeonyesha haimhitaji kwa zaidi ya miezi miwili sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic