May 20, 2013




Waziri kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amezungumza leo bungeni na kuwataka wasanii waache unafiki.

Pamoja na hivyo, Sugu ambaye amemaliza kuzungumza dakika 10 zilizopita, amesema anacholilia Layd Jaydee leo, ndicho walichokipigania wao tokea mwanzo.

“Anachokipigania leo Lady Jaydee ndicho walichokuwa wakipambana Vinega kukipata, lakini badala yake wakaonekana ni kama wasaliti.

“Ilifikia wakati tukaonekana kama tumepewa fedha kudai haki yetu, kitu ambacho hakikuwa sahihi,” alisema Sugu ambaye ni Mbunge wa Mbeya mjini.


“Wasanii waache uoga na unafiki na kurudi katika mstari na kuanza kudai haki zao.”

Awali Spika, Anna Makinda alijaribu kumzuia Sugu kuzungumza hasa alipogusia suala la Daudi Mwangosi.

Lakini Sugu aliendelea kuzungumza licha ya vipasa sauti kuzimwa hadi pale vilipowashwa na akaendelea kuzungumza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic