May 11, 2013




 Kocha André Villas-Boas wa Tottenham ameamua kufunguka na kusema anataka kumsajili mshambnuliaji David Villa wa Barcelona.

Spurs imetenga kitita cha euro milioni 8.5 ili kumnasa Villa ambaye amekuwa hana msimu mzuri na klabu hiyo, lakini taarifa nyingine zimeeleza klabu hiyo ya Catalan inataka kitita cha euro milioni 14.


Tayari Villa amewekwa sokoni na Barcelona na hiyo inatokana na kuonyesha Kocha, Tito Vilanova kutomhitaji kwa kiwango kikubwa.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 31 ameeleza yuko tayari kutua England lakini atalazimika kusubiri makubaliano ya Barcelona na Spurs kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic