May 10, 2013




Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameendelea kulinogesha pambano la watani la Mei 18 baada ya kusema maneno yaliyotolewa na Wazee wa Yanga, hata kwenye kanga yapo.

Wazee wa Yanga wakiongozwa na Mzee Akilimali aliyekuwa akizungumza kwa niaba ya Alhaji Jabir Katundu walisema Simba haina ujanja, lazima ifungwe Mei 18.


Wazee hao walitumia neon la “Mnyama lazima afe” wakati wakizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Lakini Julio amesema majigambo ya wazee hao ni maneno tu ambayo hata katika kanga ambalo ni vazi la kinamama, yanapatikana.

“Sisi tunaendelea vizuri na maandalizi na si lazima kuweka kambi, inawezekana ikawepo au isiwepo.

“Kesho (Jumamosi) tunaweza tukawa tumepata jibu, lakini tunashirikiana vizuri na kocha mkuu kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri,” alisema Julio.

“Maneno waliyosema Wazee wa Yanga, hata kwenye kanga yapo. Mpira na maneno ni vitu tofauti, sisi tunafanya maandalizi na wasidhani kila kitu kitakuwa mchekea.

“Nilishasema mara nyingi kuhusiana na Yanga, nimeifunga mara nyingi nikiwa mchezaji hata nikiwa kocha,” alisema Julio.

Pambano hilo awali lilionekana kama halina msisimko, lakini ushindi mfululizo wa mechi tatu huku Simba ikionyesha kiwango kizuri, imeamsha hamasa kubwa.

Hali ambayo imefanya asilimia kubwa ya watu kutaka kuliona pambano hilo la Mei 18 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic