Real Madrid wamewatambia wapinzani wao Barcelona kwa upande wa mpira wa kikapu kwa kuwachapa na kufanikiwa kutinga katika fainali ya Kombe la Ulaya.
Mchezo huo wa fainali utacheza kesho Jumapili mjini Londona ikiwa ni baada ya Madrid kuvuka kwa kuichapa Regal Barça vikapu 67-74.
Madrid maarufu kama Los Blancos walizidia Barca wanaojulikana kama Catalans kila idara na hadi mwisho wa robo ya kwanza walikuwa wanaongoza vikapu 20-4.
Kutokana na ushindi huo sasa Madrid watawavaa Wagiriki, Olympiacos Jumapili mjini London.
Wagiriki hao waliwang’oa waliokuwa mabingwa CSKA Moscow kwa kuwachapa vikapu 52-69. Fainali hiyo inatarajiwa kuwa ngu na yenye ushindani wa hali ya juu.
Mashabiki wa Madrid waliingia mtaani baada ya mchezo huo na kuimba wakishangilia kuonyesha kikosi chao kilikuwa ni cha mashujaa.
Mchezaji Marcelinho Huertas ndiye aliongoza kwa kufunga vikapu 19 kwa Barcelona wakali mkali kwa Real Madrid katika mchezo huo alikuwa Felipe Reyes aliyetikiza vikapu 17.
0 COMMENTS:
Post a Comment