May 10, 2013


Yanga wakiwa mazoezini jijini Dar es Salaam..


Mabingwa wapya wa soka Tanzania, Yanga wameanza kambi mjini Pemba kujiandaa na mechi yao ya kufunga msimu dhidi ya watani wao Simba Mei 18 jijini Dar.

Yanga ikiwa tayari bingwa, imetangaza kutaka kushangilia ubingwa wao vizuri siku hiyo kwa kuifunga Simba kwa kuwa wanajua ni siku watakayokabidhiwa kombe.

Pamoja na Yanga kufanya siri kubwa kuhusu kambi hiyo, mmoja wa viongozi wake aliiambia Salehjembe: 


“Kambi itakuwa Pemba kwa kuwa kuna sehemu tulivu sana,” alisema.
Lakini Simba wamekuwa wakitaka kushinda ili kupata nafasi ya tatu ili kuepuka ligi wakiwa nafasi ya nne.

Ukiachana na hivyo, Simba wanataka kuendelea kuwanyima raha Yanga kwa kuwa mara ya mwisho kukutana nao msimu huu ilikuwa sare ya bao 1-1.

Lakini mechi ya kufunga msimu uliopita, Simba waliitandika Yanga kwa mabao 5-0, kitu ambacho kimekuwa kikiwaumiza sana mashabiki wa Yanga.

Kambi hiyo ya Yanga visiwani humo inaonyesha wamepania kushinda mechi hiyo ingawa ni mabingwa.

Tayari wazee wa klabu hiyo wamesisitiza lazima watashinda mechi hiyo ya Jumamosi ijayo.

Yanga imekuwa ikitaka kushinda wakati Simba wamekuwa wakisisitiza hawana la kupoteza na siku hiyo watatoa burudani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic