Mazoezi ya Yanga yameendelea
kuwa kivutio mjini Pemba kutokana na watu wengi kujitokeza kuyaangalia.
Pamoja na hivyo, mashabiki
wengi wanaojitokeza katika Uwanja wa Gombani, wameonyesha kuridhishwa na kiwango
wanachokionyesha Yanga.
Mazoezi hayo chini ya Mholanzi,
Ernie Brandts yamekuwa yakiwavutia watu wengi na kujenga imani zaidi.
Mashabiki wengi wa Yanga
waliopata nafasi ya kuona mazoezi hayo wamekuwa wakijenga imani kwamba lazima
Simba italala katika mechi ya Mei 18.
Wengi wanaamini Simba
itafungwa kwa kuwa wachezaji wanaonekana wako katika hali nzuri zaidi.
Lakini Yanga wameonyesha
asilimia kubwa ya mazoezi yao kuwa siri wakihofia hujuma.
Yanga imeweka kambi mjini
hapa na kuzua gumzo huku baadhi ya mashabiki wakionyesha kufurahishwa na uamuzi
wa Yanga kuweka kambi Pemba wakati Simba wako Unguja.
0 COMMENTS:
Post a Comment