Rais wa Real
Madrid, Florentino Perez amekata mzizi wa fitina na habari za tetesi baada ya
kusisitiza kwa mara nyingine kwamba Cristiano Ronaldo hatakwenda Manchester
United au timu nyingine yoyote.
Perez amewaambia
waandishi mjini Madrid leo kwamba Ronaldo hatahama kwenda Manchester United
wala timu nyingine.
“Nafikiri
tufunge mjadala wa Ronaldo, maana hatahama, Manchester wanalijua hili na sasa
wanaendelea na mambo mengine.
“Sisi tunaanza
mipango ya mambo mengine, hivyo Ronaldo bado yupo nasi, pia analijua hilo,”
alisema.
Kauli hiyo ya
Perez inakata kabisa kiu ya mashabiki wa Man United waliokuwa wanatamani
Ronaldo arudi katika klabu hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment