URA ya
Uganda iliivaa Simba jijini Dar es Salaam na kiungo mshambuliaji wake wakati
huo, Haruna Moshi ‘Boban’ alikuwa tatizo kubwa kwa beki huyo Mganda.
Pamoja na
kumtoka mara kadhaa, lakini Boban alifanikiwa kupiga krosi kadhaa baada ya
kumtoka Ssenkoomi wakati wa mechi hiyo ya Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam kama picha zinavyoonyesha.
Ssenkoomi
sasa amejiunga na Simba akitokea URA wakati Boban ameondoka Simba na kwenda
kujiunga na Coastal Union ya Tanga atakayoitumikia msimu ujao.
Huenda wawili
hao wakakutana tena kwa mara nyingine katika mechi mbili za msimu ujao.
0 COMMENTS:
Post a Comment