Beji aliyokuwa
ameivaa mmiliki wa Sunderland, Ellis Short wakati akimkaribisha Rais Jakaya
Kikwete katika klabu yake imezua mjadala nchini Uingereza.
Beji hiyo
yenye maneno FTM ni maarufu kama sehemu ya kuwadhihaki wapinzani wakubwa wa
Sunderland klabu ya Newcastle.
Lakini vyombo
vya habari vimeichambua kama beji hiyo hiyo, dhihaka zake ni za matusi hivyo
haikuwa sahihi Short kuivaa wakati akimtambulisha mambo kadhaa ya klabu yake
Rais Kikwete.
Maelezo ya
mtandao mmoja wa Uingereza yameeleza, imefikia wakati watoto wanapotaka kununua
beji hiyo au wakiulizia maana yake katika duka la kuuza vifaa vya Sunderland
wamekuwa wakibadilishiwa maana.
Lakini Short
aliwahi kununua sita kutoka katika duka hilo na kuahidi kuwa anazivaa katika
sehemu maalum na inaonekana moja wapo alichangua hiyo alipokutana na Rais
Kikwete.
Beji hiyo
ya FTM imekuwa ikitumika kama dhihaka kwa Newcastle ambao ndiyo wapinzani
wakubwa wa Sunderland kwa kuwa timu zote zinatokea mji mmoja wa Sunderland.
Rais
Kikwete ambaye aliwaunganisha Simba na club hiyo, siku chache zilizopita alikuwa
mjini Newcastle kutembelea klabu hiyo ya Sunderland.
Steve Wraith ambaye ni mhariri mkuu wa NUFC, maana hasa ya FTM ni “Follow The Mackems”, ikiwa ni maana ya nendeni mkapambane na Mackems na si vinginevyo.
“Lakini maana hiyo imebadilishwa na kuwa kama tusi, lakini si kweli. Hivyo sioni kama kuna sababu ya mashabiki wa Newcastle kuanza kupambana na Short katika hilo,” alisema Wraith
0 COMMENTS:
Post a Comment