Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig
amesema uongozi wa klabu hiyo umekubali kumlipa fedha zake.
Liewig raia wa Ufaransa ameiambia Salehjembe
kwamba alifanya mkutano na Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage na amekubali
kulipa fedha zake mishahara ya miezi miwili na nusu pamoja na miezi miwili
mingine ambayo inaingia katika kuvunja mkataba.
Liewig alikuwa analipwa dola 6,000 kila mwezi,
maana yake anaidai Simba kitita cha dola 27,000.
“Kweli wamekubali, lakini sijajua kuhusiana na
utekelezaji. Naendelea kusubiri hadi mambo yatakapokuwa mazuri.
“Nitafurahi wakitekeleza ahadi kwa kuwa sikuja
hapa kugombana na mtu, vizuri wakinilipa halafu niondoke kwa amani. Hadi sasa
ninawaamini ndiyo maana nasubiri,” alisema Liewig.
Hata hivyo kuna taarifa Simba inataka kulipa
kiasi tu cha fedha hizo halafu iandikishiane na kocha huyo ili iendelee kumlipa
taratibu.
0 COMMENTS:
Post a Comment