June 24, 2013




Mshambuliaji nyota wa Napoli, Cavani amepanga siku rasmi ambayo ataamua iwapo anabaki au anaondoka zake katika klabu hiyo.

Inaonekana siku ambayo atapanga Cavani kuondoka basi safari yake itaishia Real Madrid lakini yeye amesema Julai 20 ndiyo atatangaza rasmi.

Akizungumza katika mahojiano na Radio Rai ya Italia, Cavani ambaye yuko nchini Brazil na kikosi cha timu yake ya taifa ya Uruguay kinachoshiriki michuano ya Kombe la Mabara alisema anategemea kutoa uamuzi wake siku hiyo.


Hivyo kuwataka watu watulie na kumuacha aendelee kutafakari na mwisho aamue kuhusiana na safari yake hiyo.

Kwani Real Madrid, Chelsea na Man City ni kati ya klabu zinazomhitaji ingawa dalili zinaonyesha anaweza kwenda Hispania.

Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amesisitiza kuwa anaamini mshambuliaji wake huo ataendelea kubaki Napoli na kuziacha wazi klabu zinazomuwania kwa kasi kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic