Vijana Watanzania walio mjini hapa, leo
wameendelea na mafunzo kuhusiana na mchezo wa soka.
Vijana hao chini ya Fels Project
wamekuwa wakifanza mafunzo mbalimbali ikiwemo lugha, kujifunza suala la
kuheshimu muda, kusikiliza mafunzo pamoja na mpira.
Vijana hao walifanya mazoezi chini ya
Kocha Alex ambaye aliwafundisha namna ya kufunga na kuzuia, lakini namna mpira
unavyomilikiwa kwa kufuata mafunzo.
Pamoja na hivyo, walicheza na baadhi za
watoto ambao wanaendelea kuchukua mafunzo ya soka ambao umekuwa ni mfumo wa
nchi za Ulaya kuwakuza watoto wakianza na mafunzo mapema.
0 COMMENTS:
Post a Comment