Kocha wa
zamani wa Simba, Talib Hilal hivi karibuni alifanya mafunzo ya mchezo wa soka la
ufukweni katika nchi ya Guam.
Talib
aliyewahi kuipa Simba ubingwa mwaka 2008, aliongoza mafunzo hayo kwa lengo la
kuboresha mchezo huo unaochipukia kwa kasi.
Kocha huyo
ambaye sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Oman pamoja na mkufunzi wa Shirikisho
la Soka la Kimataifa (Fifa) amekuwa akifanya mafunzo katika nchi mbalimbali duniani.
“Nimemaliza
na Guam, jamaa wamepata faida na nchi yao ni sawa na mkoa mmoja tu kama
Morogoro. Lakini sisi nyumbani (Tanzania) bado tumelala na hakuna anayeonyesha
kuchangamka,” alisema.
Mwezi uliopita,
Hilal alifanya mafunzo kama hayo nchini Uganda ambayo imepania kuanza kucheza
Beach Soccer.










0 COMMENTS:
Post a Comment