Mkali
LeBron James alipiga pointi 37 na kuisaidia timu yake ya Miami Heat kushinda
kwa mara ya pili mfululizo ubingwa wa NBA.
Katika
mechi hiyo kali ya fainali dhidi ya San Antonio Spurs, mwisho Heat waliibuka na
ushindi wa pointi 95-88.
Katika
mechi za awali, Spurs walionekana kuwa na nafasi zaidi ya kuwa mabingwa lakini
Heat waliendelea kupambana hadi kulazimisha kufikia mechi ya saba ya fainali.
Katika
mechi hiyo ya leo alfajiri, Lebron pamoja na kufunga pointi 37, lakini alipata
rebound 12 na kuimaliza kabisa Spurs.
Baada
ya kucheza vizuri namna hiyo, Lebron alitunukiwa tuzo ya mchezaji bora maarufu
kama MVP kwa mara ya pili mfululizo.
Spurs
ilianza kuongoza kwa pointi 11-4 na kuonyesha ilikuwa imepania kuchukua ubingwa
lakini Heat hasa Lebron na Wade walicharuka na kubadili mambo hadi ikafikia 72
kwa Heat na 71 kwa Spurs wakati wanaanza robo ya nne ambayo ilikuwa inasubiriwa
kutoa majibu ya nani bingwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment