Na Saleh Ally, Freiburg
Vijana wa Kitanzania walio katika mafunzo ya soka na maisha leo wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Schallstadt.
Vijana wa Kitanzania walio katika mafunzo ya soka na maisha leo wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Schallstadt.
Schallstadt moja
ya timu inayosifika kwa kuzalisha wachezaji nyota ilijikuta katika wakati mgumu
kutoka kwa vijana hao wa Kitanzania.
Mabao ya
Watanzania hao wa kikosi kinachofanya mafunzo chini ya Fels Project yalifungwa
na Miraji Athumani au Sheva na Carlos Sekule.
Wakati Carlos
Protus, Rajab Rashid na Emily Josiah Mgeta wakifanya kazi ya uhakika katika
safu ya ulinzi na kumfanya kipa wao apumzike kama yuko pikniki.
Vijana hao wanaendelea na mafunzo ya soka pamoja na
maisha ya kawaida lengo likiwa ni kuwawezesha kuwa imara na uhakika wa kufanya
vizuri kama watapata timu za kucheza barani Ulaya, Afrika au kwingineo lakini
pia katika maisha ya kila siku.
0 COMMENTS:
Post a Comment