Hatimaye dalili za safari ya mwisho ya
marehemu Albert Mangweha kurejea nyumbani zimeanza kuonekana.
Tayari mwili wa Mangweha ‘Mangwea’ umetolewa
katika chuma cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya St Helen Joseph na
kukabidhiwa kwa undertaker.
Undertaker ni mtu anayefanya kazi ya
kushughulikia kumuosha, kumvisha nguo na kumpamba maiti na baadaye kumhifadhi
vizuri kwenye jeneza.
Kampuni inayofanya kazi hiyo tayari
imeuchukua mwili wa Mangwea na hiyo ni dalili kwamba ndani ya siku mbili safari
ya kurejea nyumbani itakuwa imeiva.
“Tayari undertaker ameuchukua mwili, hali
hiyo ina maanisha kwamba safari ya Dar ni ndani ya siku hizi mbili.
“Vijana hapa wanaendelea na michango na
wengine wataungana na mwili wa marehemu kuja huko nyumbani,” alisema Mtanzania
anayeishi nchini Afrika Kusini aitwaye Joseph.
“Nimeambiwa huyo undertaker ni Mtanzania,
hivyo tunaamini mambo yataenda vizuri zaidi,” aliongeza Joseph.
Tayari imeelezwa mwili wa Mangwea utawasili
nchini Jumapili jioni na Jumatatu ataangwa kabla ya kuanza safari ya kwenda
Morogoro ambako atazikwa.
Mangwea alifariki Jumanne iliyopita baada ya
kukutwa akiwa chumbani ameishakufa, huku mwenzake M To The P akiwa taabani,
hadi sasa yuko hospitali.
0 COMMENTS:
Post a Comment