June 1, 2013



 
Kipa namba moja wa Barcelona, Víctor Valdés amewaaga mashabiki wa timu yake hiyo kwa kumwaga chozi.

Valdes Amelia katika mkutano wa waandishi wa habari na kusema anaamini mechi yao dhidi ya Malaga itakuwa ya mwisho kwa kuwa mkataba wake unaisha 2014.

"Nimekuwa hapa kwa miaka ishirini, nilianza kuwa La Masía mwaka 1992, nimekamilisha miaka kumi na mbili katika timu kubwa. Nilijitolea kwa kila kitu, ni sehemu ninayoipenda lakini wakati umefika, sina namna, lazima niondoke,” alisema Valdes huku chozi likimtoka.

"Nilikuwa niongeze mkataba Januari, lakini niliona sitaweza na niliieleza klabu. Nikiwa hapa nimeshinda kila kitu, nafikiri naweza kuamua kitu kingine na mashabiki wanisamehe kwa ukimya wangu kwa kuwa niliamini siku ya kusema itafika, ndiyo leo.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic