June 1, 2013


Mshambuliaji nyota wa England, Theo Walcott amesema hajaamini macho yake baada ya kuona vijana wadogo wa shule ya msingi wakiuchezea mpira katika ufukwe wa Copacabana nchini Brazil.

Walcott ambaye ni tegemeo la ushambuliaji Arsenal, alisema vijana hao walikuwa wakiuchezea mpira katika hali ya kushangaza, kitu ambacho hakukitegemea hata kidogo.

Alisema: “Tulikwenda bichi Alhamisi, niliwaona vijana sita au saba wakiuchezea mpira kwa mabega, hakika nilichokiona hata sisi hatuwezi kukifanya kama wachezaji wa timu ya taifa.

“Nasisitiza sitawaweza wala siwezi kufikia uwezo wao kabisa, kwangu kilikuwa kitu cha ajabu kabisa.”
Walcott yuko nchini humo na kikosi cha timu ya taifa ya England tayari kuivaa Brazil katika mechi gumzo ya kirafiki itakayopigwa kesho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic