June 19, 2013



Na Saleh Ally
KIUNGO nyota we Ivory Coast, Yaya Toure ameendeleza vituko na misimamo baada ya kugoma kushuka kwenye ndege wakati wakiwa njiani kurejea jijini Abidjan.

Baada ya mechi dhidi yaTaifa Stars, Tembo hao walielekea moja kwa moja kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kuanza safari ya kwenda kwao Ivory Coast.


Wakiwa njiani, ndege hiyo iliteremka katika mji mkuu wa Benin uitwao  Porto-Novo ambako walikodi ndege hiuo, lengo lilikuwa ni kuweka mafuta.
Lakini mmoja wa mawaziri wa serikali ya nchi hiyo ambaye alipewa taarifa Ivory Coast watapita hapo, aliomba wachezaji na viongozi washuke na kuingia kwenye cchumba cha wageni maarufu ‘VIP Room’, ili wapate angalau vinywaji kidogo huku akiwa nao.


Baada ya mjadala kidogo, viongozi walikubali kuteremka, lakini Yaya akawa wa kwanza kuweka msimamo kwamba hatateremka.

“Safari yetu ilikuwa nzuri sana, ila tulipofika Benin kidogo kukawa na vituko kidogo. Waziri mmoja wa serikali ya nchi hiyo alisema tushuke, lakini ilikuwa vigumu kwa Yaya ambaye alisisitiza kwamba anafuata ratiba.

“Kweli ratiba yetu pale ilikuwa ni kuweka mafuta tu, unajua hata hiyo ndege tumeikodi pale. Nafikiri waziri huyo aliona vizuri kuwaona wachezaji hao, lakini Yaya hakushuka hali iliyofanya viongozi wabadili msimamo na kusema kushuka au kutoshuka ni uamuzi wa wachezaji wenyewe.

“Kweli wengine wakashuka, wengine baadhi nafikiri watatu au wanne akiwemo Yaya wakabaki kwenye ndege,” alisema Aziz Alibhai ambaye alikuwa kwenye msafara huo.

Akiwa jijini Dar, Yaya aligoma kutoka chumbani asubuhi siku ya mechi dhidi ya Taifa Stars na kutaka apelekewe kifungua kinywa chumbani.
Hata juhudi za kocha Sabri Lamouchi zilikwama kumtoa chumbani baada ya kusisitiza alikuwa ana ‘focus’ (anafikiria chakufanya katika mechi ya siku hiyo).

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. hahahaaaah watu wanawapenda nyota hao, lakini nyota hao wamejisahau kuwa kazi yao ni ya kuburudisha watu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic