Aliyekuwa msaidizi wa kocha wa zamani wa Real Madrid, Jose Mourinho naye ameamua kuachana na klabu hiyo.
Aitor Karanka ameondoka klabuni hapo juzi Jumatatu baada ya kumalizana na uongozi wa Real Madrid.
Karanka ambaye alirudi mara ya pili Madrid baada ya kurudishwa na Mourinho kwa mara ya pili kwani kabla aliwahi kuwa mchezaji wa timu hiyo.
Ingawa alikuwa anapewa sapoti kubwa na Rais wa Madrid, Florentino Pérez lakini Karanka ameamua kutobaki na Los Blancos.
Kisa kinaonekana ni uamuzi wa kocha mpya Carlo Ancelotti kutua na timu yake ya wasaidizi na alijua atapangwa katika sehemu ambayo haitakuwa ikimruhusu kufanya kazi za ufundishaji kitu ambacho asingependa.
Hivyo Madrid na Karanka waliingia katika makubaliano ya kimyakimya na kukubaliana vizuri, naye akaamua kuondoka.
Taarifa zinaeleza huenda Mourinho akamuita rafiki yake huyo akajiunga na benchi la Chelsea jijini London.









0 COMMENTS:
Post a Comment