Maxi Biancucchi ambaye ni binamu wa Lionel Messi anaongoza kwa upachikaji wa mabao katika Ligi Kuu ya Brazil akiwa na timu yake ya Victoria.
Katika mechi saba za ligi hiyo maarufu kama Brasileirao, katika mechi saba, Maxi amepachika mabao sita.
Maxi ni mtoto wa Marcela Cuccitini ambaye ni dada wa mama yake mzazi Messi aitwaye Celia María, Messi's mother.
Kama ilivyo kwa Messi, Maxi alizaliwa katika mji wa Rosario miaka mitatu kabla ya Messi ikiwa ni Septemba 15, 1984.
Alianza kuchipukia wakati akiwa na timu ya vijana ya San Lorenzo na baadaye akajiunga na klabu ya Paraguay ya Libertad, hiyo ilikuwa ni mwaka 2004.
Baadaye aliendelea kuhama klabu moja hadi nyingine akianzia na General Caballero, Tacuary, Fernando de la Mora, Sportivo Luqueño na Olimpia.
Baada ya hapo akaanza kupata mafanikio na kuzichea klabu kubwa za Amerika Kusini kama Flamengo (Brazil) na Cruz Azul (Mexico) kabla ya kutua Vitoria, mwanzoni mwa msimu huu.
Maxi, Messi pia wana binamu zao wengine ambao ni wanasoka na wanafanya vizuri ambao ni Emmanuel mwenye miaka 24 anayechezea Olimpia ya Paraguay. Mcheaji huyo alihamia timu hiyo baada ya kuwa na msimu usio na mafanikio katika klabu za 1860 Munich na Girona. Lakini pia yuko Bruno,14, anayecheza timu aliyochipukia Messi kisoka ya Newell.







0 COMMENTS:
Post a Comment