Jezi za mshambuliaji mpya wa Atletico Madrid, David Villa zimeshika mauzo ya juu kutokana na mashabiki kuzinunua kwa wingi.
Jezi hizo zenye jina mgongoni David Villa na namba 9 mgongoni zimekuwa kivutio kikubwa na dalili za mauzo makubwa zilionekana tokea siku ya kwanza alipotua kutambulishwa kwa mashabiki.
Villa anaonekana ni jasiri kutokana na kukubali kuchukua jezi ya wachezaji ambao walikuwa tegemeo au mashujaa wa timu hiyo.
Namba 9 katika klabu hiyo ndiyo jezi yenye heshima zaidi kwa kuwa wengi ambao ambao waliivaa walifanya vizuri wakiwa na klabu hiyo na mfano wao ni Fernando Torres, Kun Aguerro na wa mwisho alikuwa ni Radamel Falcao.
Lakini kingine kinachowavutia mashabiki ni kwamba Villa anatokea katika jiji la Barcelona na sasa anahamia Madrid na miji hiyo imekuwa ina upinzani mkubwa hadi kiutamaduni.








0 COMMENTS:
Post a Comment