July 16, 2013



Kocha Carlo Ancelotti amekutana na kiungo wake Ricardo Kaka kwa mara nyingine tena katika mazoezi ya kwanza.

Wawili hao wamekutana safari hii wakiwa katika klabu ya Real Madrid baada ya kuwa walifanya kazi kwa mafanikio makubwa wakiwa AC Milan ya Italia.

Tayari hali hiyo imeanza kuzua mjadala wengi wakiamini Ancelotti atatoa upendeleo kwa Kaka ambaye msimu uliopita hakupata nafasi chini ya Jose Mourinho.

Chaguo la Mourinho alikuwa Mesut Ozil aliyemsajili na alionyesha uwezo mkubwa.
Lakini Ancelotti amesisitiza atapanga timu kutokana na kiwango cha kila mchezaji na si uswahiba wala mazoea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic