Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wanatarajia kushuka uwanjani kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam baada ya msimu uliopita kwisha Alhamisi.
Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.
Yanga itashuka dimbani kuwavaa Pillars FC ya Nigeria ambayo inajumuisha wachezaji kutokana sehemu mbalimbali za Nigeria.
“Tutacheza na hao Wanigeria kwa ajili ya kujipima nguvu na kukipima kikosi chetu, lakini tutawakosa wachezaji walio katika kikosi cha timu ya taifa,” alisema.
Baada ya mechi hiyo dhidi ya Wanigeria, Yanga itapumzika siku mbili na Jumapili itashuka tena dimbani kuivaa URA ya Uganda.
Tayari Yanga ilianza kucheza mechi za kirafiki mikoani lakini haikuwa na matokeo mazuri na kocha Brandts alisema ilitokana na kuwakosa wachezaji wake walio katika kikosi cha Taifa Stars lakini pia viwanja vibovu vya mikoani.







0 COMMENTS:
Post a Comment