July 27, 2013


Beki Hamis Buyinza amesema anaamini angeweza kufanya vizuri katika kikosi cha Simba, lakini amegundua ndani ya timu hiyo kuna tatizo.
Buyinza amesema uongozi wa Simba umekuwa na kauli zinazokinzana, ndiyo maana ameshindwa kufanya vizuri.

Akizungumza na blog hii, Buyinza alisema aliambiwa angefanya majaribio kwa wiki mbili lakini haikuwa hivyo.

“Kilichonichanganya zaidi ni kwamba jamaa walisema nitafanya majaribio, lakini mazoezi hayakuchukua hata siku tano tayari tulianza kucheza mechi.
“Bado sikuona kama kulikuwa na suala la majaribio lakini nilikuwa nikicheza kama mchezaji wa siku zote wa Simba.


“Mimi naona Simba ni timu nzuri lakini ina watu wengi wanaofanya uamuzi wa mambo, kitu kibaya zaidi wengi hawajui mpira, hivyo wanasababisha kuwa na mvutano kwa kila jambo.

“Nimecheza Uganda nikiwa nahodha wa timu kubwa kubwa, nimecheza Vietnam na hata timu ya taifa ya Uganda. Sasa kusema siwezi kabisa ni kitu cha ajabu sana.

“Angalia walisema Derrick (Walulya) si mchezaji mzuri, lakini leo yuko anafanya vizuri na URA. Kweli nilitaka kucheza Simba ila nimesikitika sana,” alisema.


Beki huyo aliyekaribishwa kwa mbwembwe jijini Dar na kuanza mazoezi na Simba alitupiwa virago vyake na kutakiwa arejee kwao na amefanya hivyo sambamba na beki mwingine Ssenkoomi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic