MOSHA AKIWA NA MWANAYE EDGAR KATIKA STUDIO ZA VOA JIJINI WASHINGTON, USA |
Mtoto Edgar Davis Mosha amepata nafasi kubwa ya kufanya majaribio katika klabu kubwa ya England ya Chelsea.
WAKIWA NA WATANGAZAJI WA VOA JULIET NA SUNDAY SHOMARI |
Chelsea ndiyo mabingwa wa Kombe la Europa na Edgar ambaye ni mtoto wa Davis Mosha ambaye ni mfanyabiashara na makamu mwenyekiti wa zamani wa Yanga atafanya majaribio katika klabu hiyo baada ya kuvutiwa na kipaji chake.
Mosha ameliambia Shirika la Habari la Sauti ya Amerika la VOA kuwa Edgar amepata nafasi hiyo baada ya kuonyesha kipaji chake cha hali ya juu.
Kiongozi huyo wa zamani wa Yanga ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Delina amesema mwanaye amepata nafasi hiyo nchini Uingereza walipokuwepo kwa kuwa ni mwanafunzi wa masomo ya soka.
WAKIWA NA SUNDAY SHOMARI NJE YA JENGO LA VOA |
Ingawa hajaeleza majaribio hayo ni lini lakini imeelezwa ni hivi karibuni na klabu hiyo ya England pia ina mchezaji Mtanzania Adam Nditi.
PICHA NA SWAHILITV.BLOGSPOT.COM
0 COMMENTS:
Post a Comment