July 1, 2013



 Na Saleh Ally
Kiungo nyota wa zamani Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ na beki Juma Nyosso wataanza maisha mjini Tanga kwa kuishi kwenye nyumba ambayo imewekewa ‘AC’ au kiyoyozi kwa muda wote watakaokuwa mjini Tanga.

Uongozi wa Coastal Union, umesema umeamua kukodisha hoteli moja maarufu ya mjini humo ambayo iko kwenye ufukwe na kuifanyia ukarabati wa hali ya juu.

Mdhamini Mkuu wa Coastal Union, Mohammed Bin Slum amesema, kila chumba katika hoteli hiyo itakuwa na kiyoyozi na ndani yake kutakuwa na ukumbi maalum wenye michezo mbalimbali.

“Wachezaji wataishi katika hoteli hiyo ya nyota tano na ukarabati uko katika hatua za mwisho. Tumeamua pia kuwawekea michezo mbalimbali kama pool, tenisi na plays station ili kuwafanya watulie wanapokuwa pale,” alisema Bin Slum.


“Lakini kutakuwa na tv sehemu maalum kwa ajili ya wao kupata nafasi ya kuona mechi mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa.  Lengo ni kuwafanya wachezaji wawe katika hali ya utulivu na vizuri zaidi makocha na benchi la ufundi wataishi hapo.”

Alipoulizwa sababu ya kubadili mfumo wa misimu iliyopita ambayo baadhi ya wachezaji walikuwa wamepangiwa nyumba, alisema:

“Mwisho tumeona si sahihi, maana kuna baadhi ya wachezaji hawakuwa waaminifu. Sisi tuliwaamini kama professional lakini wao wakatuangusha na wengi wakatoroka usiku kwenda kufanya starehe na mambo ya wanawake. Sasa tumeamua kutumia mfumo mwingine.”

Boban na Nyosso wamekuwa gumzo kubwa baada ya kuamua kujiunga na Coastal Union kwa ajili ya msimu ujao baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na uongozi wa Simba.

Boban alijiunga na Coastal Union baada ya uongozi wa Simba ‘kumkaushia’ wakati Nyosso aliamua kuvunja mkataba na kutua zake kwa Wagosi wa Kaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic