July 14, 2013





Pamoja na ushindi mfululizo mikoani, Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni amesema kikosi chake kinahitaji mechi zaidi za kimataifa.

Kibadeni anayesaidiwa na Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema mechi za mikoani zimemsaidia kujua mambo kadhaa muhimu kwake lakini angependa kuona wanacheza mechi zaidi na hasa za kimataifa.

“Mikoani kumetusaidia sana, kwanza tumecheza katika mazingira ambayo si mazuri lakini ndiyo tunalazimika kujifunza kwa kuwa baadhi ya mechi tutacheza huku.



“Lakini mechi zaidi na hasa za kimataifa zitatusaidia zaidi kwa ajili ya kujijenga zaidi,” alisema.

Tokea imetua Tabora, Katavi na Kahama mkoani Shinyanga, Simba imekuwa ikiendeleza vipigo kwa kila timu wanayokutana nayo.

Tayari Simba imeandaliwa mechi ya kirafiki ya kimataifa na itacheza na URA kutoka Uganda, mechi itakayopigwa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic